2 Julai 2025 - 13:27
Source: Parstoday
Iran yarekodi mauzo ya nje yenye thamani ya dola bilioni 11.6 katika msimu wa machipuo

Mauzo ya nje ya Iran yasiyo ya mafuta katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka wa Kiiran yalifikia tani milioni 34 na 476 elfu, zenye thamani ya dola bilioni 11 na 655 milioni.

Kiasi hiki cha bidhaa zilizosafirishwa nje kilipungua kwa 9.3% ya uzito na 14.4% ya thamani ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Katika kipindi hiki, tani 11,133,000 za bidhaa za petrokemikali zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 4.684 ziliuzwa nje ya nchi, ikiwa ni upungufu wa 28.7% ya uzito na 24.5% katika thamani.

Miongoni mwa mauzo matano makubwa yasiyo ya mafuta katika kipindi yalikuwa  ni propaani (gesi ya fueli), lami na gesi ya butani.

Miongoni mwa nchi ambazo zilikuwa sehemu saba kuu za mauzo ya nje ya Iran ni  China (dola bilioni 3.511), Iraq (dola bilioni 1.905), Umoja wa Falme za Kiarabu (dola bilioni 1.592), Uturuki (dola milioni 937), Afghanistan (dola milioni 510), Oman (dola milioni 437), na Pakistani (dola milioni 420).

Aidha kwa mujibu wa taakwimu, katika kipindi cha msimu wa machipuo, tani milioni 9 na 13 elfu za bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 13 na milioni 29 ziliagizwa kutoka nje, ikiwa ni 4.35% pungu kwa uzito na 11.73% kwa thamani ikilinganishwa na mwaka jana.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha